M

AkauntiKupungua kwa thamani ya Mali isiyoshikika

Fomu hii inaruhusu kubadili jina la akaunti ya ndani ya Mali isiyoshikika - Kupungua kwa thamani.

Ili kufikia fomu hii, nenda kwa Mpangilio, kisha Jedwali la Kasma, halafu bonyeza kitufe Hariri kwa akaunti ya Mali isiyoshikika - Kupungua kwa thamani.

Fomu inahusisha maeneo yafuatayo:

Jina

Jina la akaunti. Jina la kawaida ni Mali isiyoshikika - kupungua kwa thamani lakini linaweza kubadilishwa jina.

Kasma

Weka kasma ya akaunti ikiwa unataka

Kundi

Chagua kundi kwenye Kasma Taarifa ya Mapato na Matumizi ambako akaunti hii inapaswa kuwasilishwa.

Bofya kitufe cha Sasisha ili kuhifadhi mabadiliko yako.

Akaunti hii haiwezi kufutwa, inajiwekea yenyewe kwenye Jedwali la Kasma unapokuwa na angalau ingizo moja la kupungua kwa thamani.

Kwa maelezo zaidi tazama: Maingizo ya kupungua kwa thamani